Microsoft amefanya maboresho kwenye emails za Outlook - a podcast by Apollo

from 2020-05-12T17:34:02

:: ::

Microsoft ameamua kufanya maboresho kwenye Outlook ili kuweza kupambana na soko la email hasa ukilinganisha Gmail mwaka huu pia ilifanyiwa maboresho na Google katika kuipa nafasi nzuri ya kiushindani katika kipindi hiki ambacho watu Google na Microsoft zinashindana kuhakikisha zinapata watumiaji wengi.

Maboresho hayo ni kuzuia "Reply to all" isilete kero endapo ukiwa kwenye email yenye watu wengi; Outlook mails zitaweza kutuma email baadae kutokana na muda utakaopendelea (Send Later option); na pia Outlook inaweza kukupa mawazo ya sentensi za kujibu kuendana na email ilivyo ili ikurahisishie kujibu email haraka endapo ukiwa una shughuli nyingine za kufanya.Endelea kufuatilia Podcast hii ya Swahili Tek kupata taarifa nyingi na updates mbalimbali za Teknolojia. Karibu sana!!!

Further episodes of Swahili Tek

Further podcasts by Apollo

Website of Apollo